Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > Waziri Mkuu wa Ethiopia kufanya ziara nchini Eritrea.

Waziri Mkuu wa Ethiopia kufanya ziara nchini Eritrea.

Waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ameanza ziara ya kihistoria huko Eritrea siku chache baada ya nchi hizo mbili kutangaza kusitisha uhasma baina hayo.

Ethiopia na Eritrea zimewahi kupigana katika siku za nyuma kutokana na mzozo wa mpakani na tangu hapo wamekuwa na uhasama wa zaidi ya miaka 20.

Hivyo waziri mkuu, Abiy Ahmed, atakuwa wa kwanza kutembelea Eritrea katika kipindi hicho cha miongo miwili.

Mapema mwezi huu Ethiopia ilipokea ujumbe kutoka Eritrean ulioashiria heri njema baina yao.

Kiongozi wa Eritrea, Isayas Afewerki, alikuwa wa kwanza kuchukua hatua ya mawasiliano na utawala wa Addis Ababa baada ya kusifia hatua za mageuzi ya kisiasa yanayofanywa na waziri mkuu Abiy Ahmed.

Eritrea ilijinyakulia uhuru wake mwaka 1993 kutoka kwa Ethiopia lakini haikupita zaidi ya miaka mitano, mzozo baina yao ukazuka kuhusu kipande cha ardhi kame iliyompakani mwa mataifa hayo na kusababisha uhasama huo wa miongo kadhaa.

Uchunguzi wa umoja wa mataifa ulibaini kuwa kipande cha ardhi kilichokuwa kinazozaniwa ni cha Eritrea, uamuzi ambao Ethiopia haujaukubali kikamimilifu.