Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Watafiti waombwa sababu za wanaume kutokutaka kupima ukimwi.

Watafiti waombwa sababu za wanaume kutokutaka kupima ukimwi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na atoto nchini Tanzania, Dk. Faustine Ndugulile, amewataka watafiti wa afya nchini kufanya utafiti, ili kubaini sababu na suluhisho kuhusu uwepo wa idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupima virusi vya Ukimwi (HIV).

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016/17, ulioangalia maambukizi mapya na kiwango cha kufubaza VVU, wanawake wanaoongoza katika maambukizi mapya, lakini ni wepesi kupima na kutumia dawa kikamilifu ikilinganishwa na wanaume.

“Lengo hasa tunahitaji kuona idadi kubwa ya wanaume ikijitokeza kupima VVU ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi mapya ifikapo 2030. Ili tuweze kufanikisha hili, ni lazima tuwe na majibu ya kitafiti yatakayotupa mwongozo kuhusu sababu za wanaume kukwepa kupima VVU na nini hasa kifanyike kuondoa changamoto hizo,” alisema.

Kuhusu suala la upatikanaji wa dawa hapa nchini, DK Ndugulile alisema; “Kwa sasa Serikali imetoa mwongozo wa utoaji wa dawa ambapo badala ya kuruhusu soko liamue dawa gani zitumike, kwa sasa serikali ndiyo inaamua dawa ipi itumike kutibu ugonjwa upi, sehemu gani na kwa utaalamu gani.”

Moja kati ya vituo vya kupimia Ukimwi mkoani Tanga-Tanzania.

Alishukuru shirika la Swiden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huo