Sunday, April 21, 2019
Swahili > Habari > Wanawake Saudia wasubiri kwa hamu kuendesha magari

Wanawake Saudia wasubiri kwa hamu kuendesha magari

wanawake waendesha SAUDIA

Saudi Arabia imetangaza tarehe ambayo wanawake wataruhusiwa kuanza kuendesha magari katika nchi hiyo ya kifalme.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imesema, tarehe 24 mwezi Juni ndio siku ambayo marufuku hiyo ya miongo kadhaa ya wanawake kutoendesha magari itaondolewa rasmi.

Uamuzi huo uliotangazwa mnamo mwaka jana, ndio wenye mvuto zaidi katika vyombo vya habari katika mambo yanayofanyiwa marekebisha nchini humo.

Tayari, shule maalumu za kufundisha madereva vimeanza kufungulia katika sehemu mbalimbali nchini Saudi Arabia ikiwa ni maandalizi ya kuwaandaa wanawake kushika usukani.

Wakati huo huo, hofu ya kupoteza ajira imetanda miongoni mwa wageni waliopo nchini humo ambao wamekuwa wakijipatia ajira za udereva. Wengi wanahisi, mabadiliko yanayofanyika nchini humo, huenda ikiwa ndio chanzo cha wao kupata ajira.