Sunday, April 21, 2019
Swahili > Elimu > Wanafunzi wa Kidato cha 4 Waanza Mtihani Kenya

Wanafunzi wa Kidato cha 4 Waanza Mtihani Kenya

Mtihani wa Kitaifa Kenya

Watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE nchini Kenya wameanza kufanya mtihani huo hii leo.

Mtihani huo unaoshirikisha zaidi ya watahiniwa 615,000 umeanza kwa masomo ya vitendo (practicals) hadi tarehe 2 mwezi ujao wa Novemba.

Aidha mtihani huo wa kidato cha nne kwa masomo ya nadharia utaanza rasmi tarehe 6 mwezi ujao hadi tarehe 29 mwezi huo huo.

Juma hili watahiniwa hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa masomo ya lugha kama vile kijerumani, kiarabu,kifaransa na somo la muziki.

Hata hivyo, mtihani wa sayansi ya nyumbani maarufu kama Home Science uliotarajiwa kufanyika Alhamisi ya wiki hili umeahirishwa hadi mnamo Jumatatu wiki ijayo kwa sababu ya marudio ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Alhamisi hii Oktoba 26.