Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Wanafunzi UDSM wafariki kwa ajali ndani ya ambulance.

Wanafunzi UDSM wafariki kwa ajali ndani ya ambulance.

Wanafunzi wawili wa chuo Kikuu cha Dar Es Salaam pamoja na Dereva wao wamefariki dunia jana jumatatu, katika ajali iliyotokea eneo la River Side, Mabibo ikilihusisha gari la kubebea wagonjwa ( Ambulance ) na lori la mizigo.

Wanafunzi hao walikuwa kwenye gari la wagonjwa ikidaiwa walikua wakipelekwa Hospitali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( DARUSO ) imeeleza kuwa Maria Gordian, alikua mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo na Steven Sango, alikua mwaka wa pili .

Mwanafunzi mwingine aliyekua kwenye gari hiyo iliyopata ajali ni, Abishai Nkiko hali yake ni mbaya na anapata matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .

” Tuendelee kumuombea apate kupona haraka “, imesema taarifa hiyo .