Monday, June 14, 2021
Swahili > Habari > Waislamu waanza mwezi mtukufu wa Ramadhan

Waislamu waanza mwezi mtukufu wa Ramadhan

Waislamu waanza Ramadhan

Waislamu duniani kote hii leo wameanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Nchini Kenya, tangazo la kuandama kwa mwezi limetolewa na Kadhi Mkuu wa nchi hiyo Shariff Ahmed Muhdhar hapo jana jioni katika ofisi za Tume ya Wakf mjini Mombasa baada ya mwezi kuonekana mjini humo na maeneo mengine ya Afrika pamoja na mashariki ya kati.

Kadhi Mkuu alithibitisha kuonekanwa kwa mwezi na waislamu waaminifu hivyo kutangaza rasmi kuandama kwa mwezi na kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wakati huo huo, amewahimiza waislamu kuutumia mwezi huu mtukufu kwa kusaidia watu hasa waathirika wa mafuriko ya mvua nchini kote.

Pia, amewataka waislamu kujiepusha na kufanya maasi na kuishi kwa kufuata muongozo wa mafundisho ya dini, huku akitaka vyombo vya usalama kudumisha ulinzi.