Wednesday, August 21, 2019
Swahili > Habari > Wahamiaji haramu wa toka Afrika kufukuzwa Israel

Wahamiaji haramu wa toka Afrika kufukuzwa Israel

Habari

Mamlaka ya Israeli kuanzia siku ya jumapili ilianza kusambaza barua kwa maelfu ya wahamiaji wa Afrika, wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo kuwataka kuondoka hadi kufikia mwisho wa mwezi ujao.

Msemaji wa idara ya uhamiaji ya Israel ameliambia shirika la habari ya ufaransa AFP kuwa ambao watakaidi amri hiyo watakamatwa na kufungwa gerezani.

Mwezi Januari Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyah, alitangaza kuanzishwa kwa mpango wa kuwaondowa wahamiaji haramu wapatao thelathini na nane elfu.

Wengi wa wahamiaji wa Afrika wanatoka Eritrea na Sudan. Wengi wanasema wamekimbia vita, matatizo mbalimbali ya kiuchumi  katika nchi zao.

Wahamiaji, ambao baadhi yao wamekuwa wakiishi Israeli kwa miaka mingi, wana kazi lakini wanalipwa vibaya, kazi ambazo Waisraeli hawataki..

Benjamin Netanyahu alisema kuwa uwepo wa wahamiaji nchini Israel ni tishio kwa Waisrael.