Sunday, April 21, 2019
Swahili > Afya > Uvutaji wa sigara ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo na kiharusi

Uvutaji wa sigara ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo na kiharusi

Afya

Matumizi ya sigara yaongezeka kwa kasi sana duniani na wavutaji wako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la utafiti wa masuala ya afya la BMJ.

Watu wanovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 50 zaidi kupata magonjwa ya moyo na wanauwezekano wa asilimia 30 wa kupatwa na kiharusi kuliko watu amba hawavuti sigara.

Magonjwa wa moyo na saratani,yanachangia vifo kwa asilimia 48 duniani na sababu ikiwa ni uvutaji sigara na tumbaku

Afya
Wanawake, wako katika hatari zaidi kwa asilimia 57 wanaweza kupata ugonjwa wa moyo na asilimia 31 kupata kiharusi.

Utafiti huo umesema kuwa wanaume wanaovuta sigara moja kwa siku wanauwezekano wa asilimia 48 wa kupata ugonjwa wa moyo na wanauzekenao wa asilimia 25 wa kupata kiharusi.

Wanawake, wako katika hatari zaidi kwa asilimia 57 wanaweza kupata ugonjwa wa moyo na asilimia 31 kupata kiharusi.

Wale watakao acha kabisa kuvuta sigara wanaweza kupunguza kwa haraka zaidi hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.