Friday, August 14, 2020
Swahili > michezo > Urusi v/s Saudi Arabia,kitaeleweka jioni ya leo-kombe la dunia 2018

Urusi v/s Saudi Arabia,kitaeleweka jioni ya leo-kombe la dunia 2018

Saa kadhaa zimesalia kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi. Leo hii katika mchezo wa ufunguzi, wenyeji timu ya taifa ya Urusi itashuka dimbani kuikabili timu ya taifa ya Saudi Arabia.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 12:00 jioni, kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Urusi, inapigiwa chapuo zaidi ya kushinda mchezo wa leo kutokana na historia ya soka kwa timu hizo.