Sunday, April 21, 2019
Swahili > Afya > Ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaua watoto wengi wa chini ya miaka mitano

Ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaua watoto wengi wa chini ya miaka mitano

Afya

Takriban watoto milioni moja hupoteza maisha yaoa kila mwaka kutokana na homa ya mapafu

Ugonjwa wa Homa ya  mapafu  inaweza kutibiwa kwa kutumia dawa za antibiotics ambazo hugahrimu chini ya dola moja imesema ripoti ya shirika la save the Children.

Inaelezwa kuwa  ugonjwa huo umewaua watoto wengi chini ya miaka mitano kuliko  ugonjwa  wowote ule .

Nigeria, DR Congo , Ethiopia na Angola zina idadi kubwa ya vifo ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kutokana na homa ya mapafu pamoja na India na Pakistan.

Wengi wanaofariki ni watoto waliopo chini ya amiaka miwili , wengi wakiwa na kinga dhaifu iliokabiliwa na ukosefu wa chakula bora .

Shirika la save The Children limetoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa viongozi duniani kutathmini tatizo hilo la homa ya mapafu.

Pia linataka kinga zitolewe kwa  gharama ya nafua, kuwepo kwa dawa na zaidi ya watoto milioni 160 wapatiwe chanjo.