Sunday, January 26, 2020
Swahili > michezo > Tetesi za uhamisho: Madrid yamtaka Mata,Psg kumuuza Di Maria

Tetesi za uhamisho: Madrid yamtaka Mata,Psg kumuuza Di Maria

soka

Klabu ya Real Madrid inampango wa kupeleka dau kwa Manchester United ili kuweza kumsajili kiungo Juan Mata mwezi Januari,Mata anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao(Daily Express)

Psg wanamatumaini ya kuwauza  Lucas Moura na Angel Di Maria ili kuweza kununua wachezaji wangine huku wakizingia sheria ya Uefa ya kununua wachezaji kwa kujibu wa kipato cha klabu(Daily Mail)

Tottenham wanajianda kupeleka kiasi cha pauni milioni 8.8 kwa klabu ya Besiktas, ili kuweza kupata saini ya kiungo Tolgay Arslan mwenye umri wa miaka 27(Fotomac via This is Futbol)

Psg ya Ufaransa  wanaangalia uwezekano wa kumpata kocha Jose Mourinho,ili kuongeza nafasi ya kumbakisha mshambuliaji Neymar, ambae taarifa zimevuja kuwa nyota huyo anataka kutimkia Real Madrid (Don Balon via Daily Express)

soka
Mchezaji wa Leicester Islam Slimani anataka kuondoka klabuni hapo mwezi januari

Mshambuliaji wa Leicester City Islam Sliman, anataka kuondoka klabuni hapo mwezi januari na tayari vilabu vya Crystal Palace na  Rennes ya Ufaransa wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo (L’Expresion via Sport Witness)

Newcastle United wanataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Danny Ings, kutoka Liverpool haijalishi kama timu hiyo itakuwa imeuzwa au laa(Newcastle Chronicle)

Watakatifu Southampton wataangalia uwezekano mwezi januari wa kumsajili mshambuliaji Stevan Jovetic kutoka Monaco (Daily Mirror,

Mjerumani Mesut Ozil ameiambia klabu yake anaweza kusaini mkataba mpya ikiwa atapewa jezi namba kumi inayoivaliwa na Jack Wilshere(Sun)