Friday, August 14, 2020
Swahili > michezo > Senegal yaibeba Afrika, kombe la Dunia jioni ya leo.

Senegal yaibeba Afrika, kombe la Dunia jioni ya leo.

Senegal imeibuka mshindi katika mchezo wake wa kwanza leo hii kwenye michuano ya kombe la Dunia kwa kuifunga Poland magoli 2 kwa 1 , jioni ya leo .

Mkwaju wa Mbaye Niang, uliomgonga beki Thiago Cionek, uliipatia Senegal goli la kuongoza kunako dakika ya 37 ya mchezo huo. Dakika ya 60, Thiago Niang, alirudi langoni mwa Poland na kuiandikia Senegal goli la 2. Goli la kufutia machozi kwa timu ya Poland, limefungwa na Grzegorz Krychowiak mnamo dakika ya 86.

Mbaye Niang, Mfungaji wa goli la ushindi kwa timu ya Senegal.

Senegal ambayo imepangwa kundi H, imekua timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kushinda mchezo wa awali katika michuano hiyo ya kombe la Dunia,2018.