Monday, June 14, 2021
Swahili > Habari > Rais Magufuli aomboleza kifo cha Watoto Mapacha walioungana.

Rais Magufuli aomboleza kifo cha Watoto Mapacha walioungana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza msiba wa watoto mapacha walioungana, Maria na Consolata, waliofariki dunia hapo jana katika hospitali ya mkoa wa Iringa, walipokua wakipatiwa matibabu hospitalini hapo .

“Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea Taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia Taifa. Poleni familia, Masista wa Maria na Consolata na wote walioguswa, pumzikeni mahali pema wanangu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe”, ameandika Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa twitter.

Maria na Consolata, Mapcha walioungana enzi za uhai wao wakiwa darasani.

Taarifa kutoka Hospitali mkoani Iringa zinasema kuwa, watoto hao walifariki kwa muda tofauti, ambapo mmoja alifariki saa 1 usiku, na mwengine alifariki saa 3 usiku.