Tuesday, August 4, 2020
Swahili > michezo > Rage awafunda CECAFA.

Rage awafunda CECAFA.

Ismail Aden Rage,Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, amewashauri CEFACA kutoyachukulia mashindano ya CEFACA-KAGAME CUP kama bonanza na badala yake yafuate ratiba.

Kauli ya Rage imekuja baada ya baadhi ya klabu kujiondoa kutokana na ratiba ambayo haikuwa rafiki kwao ikiwemo timu ya Yanga ambayo inajiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kiongozi huyo amesema hata kama CECAFA wangeiadhibu Yanga wangekuwa wanaionea bure kutokana na mashindano yenyewe kufanyika bila kalenda maalum ambayo imekuwa haifuati uwepo wa ratiba za mashindano mengine.

Nicolas Musonya-Katibu mkuu wa CECAFA.

Ujumbe huo wa Rage, umewafikia CECAFA kupitia Katibu Mkuu wao, Nicholas Musonye ambaye yupo nchini Tanzania akisimamia michuano hiyo ya CECAFA-KAGAME CUP 2018.