Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > Polisi kenya watiwa hatiani kwa mauaji ya raia wa Uingereza.

Polisi kenya watiwa hatiani kwa mauaji ya raia wa Uingereza.

Mahakama ya Mombasa imewatia hatia polisi wa Kenya kwa kuhusika katika kifo cha Alexander Monson, raia wa Uingereza aliyeshutumiwa kutumia dawa za kulevya na ambaye alikutwa amekufa gerezani mwezi May 2012 katika mji wa Diani kusini mwa Kenya.

Kwa upande wa familia yake, wamesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alipigwa hadi kufa, huku polisi ikidai kuwa alikufa kwa kutumia kiwango kikubwa cha dawa ya kulevya aina ya Cannabis, hoja ambayo imetupiliwa mbali na mahakama.

“Kifo chake hakikuwa cha kawaida na hakikusababishwa na dawa za kulevya, maisha yake yalifupishwa na polisi,” amesema Jaji Richard Odenyo, ambaye amebaini kwamba maafisa wanne wa polisi wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji. ya Monson.

Mwendesha Mashtaka Mkuu Noordin Haji ameamuru kukamatwa kwa afisaa hao wanne wa jeshi la polisi nchini Kenya.