Sunday, January 26, 2020
Swahili > michezo > Nyota wa soka la Brazil walitamba kwa kutumia majina ya utani

Nyota wa soka la Brazil walitamba kwa kutumia majina ya utani

Nyota wengi wa Brazil, wamekuwa maarufu sana katika kusakata kandanda na umaarufu wao umekua ukiongezwa na majina wanayotumia ambayo sio majina yao halisi hawa ni baadhi ya nyota waliotamba katika soka toka nchini humo huku Jezi zao zikiandikwa majina Yao ya utani .

Marcos Evangelista de Morais ni maarufu sana kwa jina la Cafu aliwahi kutamba na vilabu vya Sao Paul, Zaragoza , As Roma na Ac Milan pamoja na timu ya taifa ya Brazil.

Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele anahesabika kama moja ya wafalme wa soka duniani aliichezea timu ya taifa michezo 92 kuanzia mwaka 1967 mpaka 1971 akifunga mabao 77.

Ronaldo Luis Nazário de Lima, alifahamika sana kama Ronaldo moja ya washambuliaji mahiri katika soka la brazil, akifunga jumla ya magoli 62 katika michezo 98 ya timu ya taifa.

Rivaldo Vitor Borba Ferreira jezi yake mgongoni ilikuwa ikipambwa na jila lake la utani Rivaldo sifa yake ikiwa ni upigaji wa mashuti ya mbali aliwahi kutamba akiwa na klabu ya Barcelona.Bebeto

José Roberto Gama de Oliveira alikuwa maarufu katika ulimwengu wa soka akiwa na jina la Bebeto ni moja kati ya washambuliaji waliotamba katika michuana ya kombe la dunia la mwaka 1994.

Manuel Francisco dos Santos, alikuwa maarufu sana kwa jina la Garrincha katika jumla ya michezo 692 alifunga mabao 276 na akiwa na timu ya taifa alifunga mabao 12 katika michezo 50.

Arthur Antunes Coimbra,kiungo mshambuliaji aliyepachikwa jila la Zico, aliitumikia timu ya taifa kuanzia mwaka 1976 mpaka 1986.

Ronaldo de Assis Moreira,yeye amekuwa maarufu kwa jina la Ronaldinho Gaúcho, mshambuliaji aliyekuwa na ufundi kwa kila aina katika soka akitamba na vilabu ya Psg, Ac Milan Barcelona aliicheza timu ya taifa michezo 97 akifunga magoli 33.

Frederico Chaves Guedes, Fred huyu ni mshambuliaji ambae hakuwa kipenzi cha wabrazil wengi japo alikuwa akipata nafasi katika timu ya taifa na akifanikiwa kufunga magoli 18 katika jumla ya michezo 39.

Antônio Augusto Ribeiro Reis,alikuwa akifahamika kwa jina la Juninho Pernambucano moja kati ya wafalme kupiga mipira iliyokufa(freekick wa) aliifungia timu ya taifa magoli sita katika michezo ya 40 aliyocheza

Ricardo Izecson dos Santos Leite, maarufu kwa jina la Kaka, alitamba sana na Ac Milan ya nchini Italia kabla ya kutua Real Madrid ,aliichezea timu ya taifa ya Brazil michezo 92 huku akikwamisha kambani jumla ya mabao 29.