Monday, January 18, 2021
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > “Nilitamani kifo” asema Wakonta .

“Nilitamani kifo” asema Wakonta .

Tangu apate ujasiri wa kupambana na hali yake na kuweza kujitafutia kipato kupitia kuandika filamu kwa kutumia simu huku akibonyeza kwa kutumia ulimi, binti Wakonta Kapunda kutoka Sumbawanga amejizolea umaarufu licha ya kuwahi kufikiria kujiua.

Wakonta, amesema kua, kipindi amepata ajali kwa bahati mbaya ilikuwa ndio kipindi madaktari walikuwa wamegoma hivyo kukaa kwa siku 20 bila kupata matibabu.

Wakonta Kapunda, akiandika kwa kutumia ulimi.

Wakonta, alisema kuwa, ”Mwaka 2012 wakati nimepata ajali, nililetwa Muhimbili lakini madaktari walikuwa kwenye mgomo kwahiyo sikupata huduma kwa zaidi ya wiki mbili ilifika wakati nikamwambia nesi mbele ya mama yangu anichome tu sindano niishie hapo”.

Aidha Wakonta ameongeza kuwa hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwake kukata tamaa ndio maana leo ameweza kuhangaika na kujipatia kipato chake kupitia kaandika filamu.

Wakonta Kapunda , akiwa amepumzika.

Wakonta alipata ajali na wanafunzi wenzake wa Kidato cha sita katika, Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, mkoani Tanga mwaka 2012 na kumsababishia ulemavu wa Uti wa mgongo “Spinal cord injury”.