Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Nape na Zitto wamkaribisha Mwigulu.

Nape na Zitto wamkaribisha Mwigulu.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Rais Magufuli kutangaza kumfuta Uwaziri aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Nape amesema anamkaribisha Nchemba kwenye maisha ya kawaida ya ubunge ili kuanza majukumu yake ya kawaida ya kuwatumikia wananchi wake waliompa kura.

Nape Nnauye-Mbunge wa Jimbo la Mtama.

“Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!“ameandika Nape Nnauye kwenye ukurasa wake wa Twitter.Nape ni moja ya wabunge wa CCM waliowahi kuteuliwa na kutumbuliwa na Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha mwaka 2015 hadi 2017.

Zitto Kabwe-Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini.

Mwingine aliyetumia ukurasa wake ni Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye ameandika, ” Karibu Ndugu yangu Mwigulu Nchemba, karibu back bench tufanye kazi ya wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT umekuponza. Ulikua msimamo madhubuti na ulisimamia haki.