Wednesday, August 21, 2019
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > habari > Mlinda amani wa tanzania auawa CAR, saba wajeruhiwa : UN.

Mlinda amani wa tanzania auawa CAR, saba wajeruhiwa : UN.

Mlinda amani mmoja kutoka Tanzania ameuawa na wengine saba kujeruhiwa kwenye kijiji cha Dilapoko eneo la Mambarika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa ametioa tarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo, ameelezea kilichotokea na hali ya majeruhi, “Tukio hilo limetokea wakati kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichokuwa katika doria kilipovamiwa na wanaodaiwa kuwa wapiganaji waliokuwa na silaha. Na kwa walinda amani saba waliojeruhiwa mmoja yuko katika hali mahtuti na anapatiwa matibabu katika hospital ya jeshi ya mpango wa Umoja wa Mataifa mjini Bangui pamoja na majeruhi wengine watatu ambao hali yao ni mbaya, na majeruhi wengine watatu waliosalia wanatibiwa Berirati.”

Ameongeza kuwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio huo. Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitafuata baadaye.