Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > Mgufuli, Kenyatta na Odinga kukutana nchini Kenya.

Mgufuli, Kenyatta na Odinga kukutana nchini Kenya.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzuru nchini Kenya mwezi ujao katika ziara ambayo itakuwa ya kihistoria.

Rais Magufuli kwenye ziara yake ataungana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga na kisha kutembelea katika Kaunti ya Nyanza.
Taarifa zinasema kuwa, Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Ijumaa ya wiki lijalo.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kuzuru nchini Kenya ni baada ya kuzuru mwaka jana ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta.
Hata hivyo, Rais Magufuli hata kabla ya kukutana na Kenyatta mwaka 2016 kwenye ziara yake nchini Kenya, mwaka huo huo alitembelewa na Raila Odinga kijijini kwake Chato..

Ziara hiyo itakuwa ni ya kihistoria na ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wawili na wenye nguvu zaidi kwenye siasa za Kenya.