Sunday, April 21, 2019
Swahili > Utalii > Meli ya Mfalme wa Oman Yawa Kivutio Zanzibar

Meli ya Mfalme wa Oman Yawa Kivutio Zanzibar

Meli ya Mfalme wa Oman

Meli hiyo yenye jina la Fulk Al Salamah ni ya Mfalme wa Oman, Sheikh Sultan Qabous bin Said itakuwa katika Bandari Kuu ya Malindi huko mjini Unguja, Zanzibar.

Meli ya Mfalme wa Omar Zanzibar
Meli ya Mfalme wa Oman ina ujumbe wa zaidi ya watu 300.

 

Ujumbe wa Meli ya Mfalme wa Oman
Ujumbe watu 300 uliopo katika Meli ya Mfalme Qabous wa Oman unaongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa nchi hiyo.

 

Meli ya Mfalme Oman
Meli hiyo inatarajiwa kutia nanga mjini humo kwa muda wa siku kumi kabla haijaelekea katika miji mengine ya pwani ya Afrika Mashariki kama zile Dar es Salaam, Mombasa, Kenya.

 

Serikali ya Zanzibar yakaribisha ujumbe wa Oman
Makamu wa rais Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akisalimiana na ujumbe wa serikali ya Oman uliowasili mjini Unguja na meli ya Mfalme wa Oman. Watu mbalimbali wamejitokeza kuangalia meli hiyo ambayo pia ina maonyesho ya vitabu na utamaduni.