Sunday, April 21, 2019
Swahili > Utalii > Meli ya Mfalme wa Oman Yatia Nanga Mombasa

Meli ya Mfalme wa Oman Yatia Nanga Mombasa

Meli ya Mfalme wa Omar Zanzibar

Meli ya kifalme kutoka Oman imetia nanga katika bandari ya Mombasa nchini Kenya ikiwa imewabeba zaidi ya watu 350 kusambaza ujumbe wa amani na uwiano kutoka kwa mfalme wa Oman.

Wajumbe hao wa Oman wakiongozwa na waziri wa mafuta na gesi Daktari Mohamed Al Rumhi na mwenyekiti wa uwekezaji SalimAl Ismaili walipokelewa na waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala na balozi wa Kenya nchini Oman Sheikh Mohamed Dor katika bandari ya Mombasa.

“Leo, tunafuraha kuwakaribisha wageni kutoka Oman, hawa ni kama jamaa zetu. Mombasa ni mji wenye ukarimu, Karibuni nyumbani.” alisema waziri Balala.

Miongoni mwa shughuli zitakazoendelea kwenye meli hio kwa muda huo wa siku nne ni kuwapa nafasi wananchi kuzuru meli hio ili kutumbuizwa na kuonyeshwa baadhi ya tamaduni za raia wa Oman.

Meli hio ilianza ziara yake katika bandari ya Zanzibar na kisha Dar es Salaam.

Yamkini meli hiyo ya kifalme itasalia katika bandari ya Mombasa kwa muda wa siku nne kabla ya kurudi Oman.