Monday, June 14, 2021
Swahili > Habari > Mbwana Samatta afanya ibada ya Hijja ndogo .

Mbwana Samatta afanya ibada ya Hijja ndogo .

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anayechezea timu ya KRG Genk ya Ubelgiji, ameenda kufanya ibada ya Hijja ndogo katika miji ya Makka na Madina. Samatta ameposti picha akiwa na mchezaji mwenzake wa KRC Genk, beki Mgambia Omar Colley wakiwa kwenye vazi maalum la ibada hiyo lijulikanalo kama Ihram katika mji wa Makka.

Mbwana Samatta akiwa Hijja na mchezaji mwenzie wa KRG Genk,Omar Colley .

Samatta amekwenda kufanya ibada hiyo baada ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu ya Ubelgiji huku akiisaidia KRC Genk kupata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zulte Waregem Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk .

Ikumbukwe ikua, Samatta ameandaa mechi maalum ya Hisani baina ya yeye na Marafiki zake, dhidi ya marafiki wa mwanamuziki Ali Kiba itakayofanyika Juni 9, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili kuchangisha madawati na miundombonu ya shule kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu.