Monday, January 18, 2021
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Magufuli achangia Tsh. milioni 10 ujenzi wa Msikiti Dar.

Magufuli achangia Tsh. milioni 10 ujenzi wa Msikiti Dar.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 600 ya simenti itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco.
Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au Mei mwakani.

Rais Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti .

“Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli