Monday, April 22, 2019
Swahili > Habari > Magaidi 15 yauwawa na Jeshi nchini Mali

Magaidi 15 yauwawa na Jeshi nchini Mali

Mali

Magaidi kumi na tano wameuwawa  nchini Mali na jeshi la nchi hiyo katika  taarifa iliyotolewa na jeshi tukio hilo lilitokea siku ya jumamosi.

Taarifa hiyo ya jeshi pia imebainisha kuwa mwanajeshi mmoja aliuwawa na wengine wawili walijeruhiwa  katika tukio hilo, tukio la kushambuliana kati ya jeshi la taifa na magaidi hao lilitokea katika misitu ya Tina iliyopoa mkoani Mopti

Katika siku za karibuni maeneo ya katikati ya nchi hiyo yamekuwa yakishuhudia mapigano makali jumaapili iliyopita ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko katika mji wa kihistoria wa Timbuktu, ilishambuliwa kwa mabomu ya moto, askari mmoja aliuwawa na wengine saba kujeruhiwa.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya  kulinda amani nchini Mali MINUSMA, na wanajeshi kutoka nchini Ufaransa  tangu  mwaka 2013 lakini bado hali ya amani haijatulia toka mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2012.