Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > Mafuriko Japani yaua watu 50.

Mafuriko Japani yaua watu 50.

Watu 50 wamekadiriwa kupoteza maisha katika mji wa Hiroshima, nchini Japan baada ya kutokea kwa mafuriko katika mfululizo wa mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Serikali ya Japan imetoa tamko la watu wanaokadiriwa kuwa milioni mbili, kuhama makazi yao kwa sababu za kiusalama.

Mafuriko ya Hiroshima nchini Japan.

Mamlaka ya hali ya hewa imeripoti kuwa mvua zinazonyesha zitasababisha athari kubwa hasa eneo la mashariki mwa Japan.
Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watu watano waliokandamizwa na mbao baada nyumba kuporomoka.

Nyumba zilivyoharibiwa na mafuriko huko Hiroshima nchini Japan.

Msemaji wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Japan ambaye ametambulika kwa jina moja Kyodo, amesema kuwa, jeshi la uhokoaji kwa kutumia ndege watazuru eneo la Okayama na Yamaguchi ambayo yameathirika zaidi.