Friday, August 14, 2020
Swahili > michezo > Mafarao wa Misri kuikabili Urusi usiku huu.

Mafarao wa Misri kuikabili Urusi usiku huu.

Muda mfupi ujao kutakua na mchezo wa kundi A katika michuano ya kombe la Dunia, ambapo wenyeji Urusi watashuka dimbani kuikaribisha Misri ” Wajukuu wa Farao “, mchezo huu unategemewa kuvuta hisia za wengi kutokana na kurejea uwanjani mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mmisri, Mohamed Salah.

Mohamed Salah, Mchezaji wa timu ya Taifa ya Misri.

Salah alikua nje ya uwanja toka Mei 26 alipoumia bega la mkono wa kushoto wakati akiipigania klabu yake ya Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid, ambapo Liverpool ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 3 kwa 1.