Monday, June 14, 2021
Swahili > Habari > Maelfu wamuomboleza kiongozi wa upinzani Msumbiji

Maelfu wamuomboleza kiongozi wa upinzani Msumbiji

Kiongozi wa upinzani Msumbiji

Maelfu ya waombolezaji nchini Msumbiji wamejitokeza katika mji wa bandari wa Beira kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wa upinzani na waasi Afonso Dhlakama aliyefariki nchini humo wiki iliyopita.

Serikali ya nchi hiyo imeamua kumpa kiongozi huyo mazishi ya kitaifa. Hii ikiwa ni kutambua uongozi wake wa chama kikuu cha upinzani, Renamo na mchango wake katika kuendesha mazungumzo ya amani na serikali.

Jeneza la kiongozi huyo, likiwa limezungushiwa bendera ya taifa, lilibebwa na wanajeshi waliokuwa wamevaa sare za kijeshi.

Kiongozi wa upinzani Msumbiji
Wakati huo huo, rais wa nchi hiyo, Filipe Nyusi, amesema yuko tayari kurudi katika meza ya mazungumzo ya amani na kiongozi wa mpito aliyechaguliwa siku ya Jumamosi.

Wakati huo huo, rais wa nchi hiyo, Filipe Nyusi, amesema yuko tayari kurudi katika meza ya mazungumzo ya amani na kiongozi wa mpito aliyechaguliwa siku ya Jumamosi.

Mpaka sasa, mamia ya wapiganaji bado wako porini baada ya chama hicho kubeba silaha dhidi ya serikali miaka mitano iliyopita.

Msumbiji bado inatibu majeraha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 16 ambavyo vilikwisha mnano mwaka 1992.

Awali, kulikuwa na hofu kwamba, kifo cha kiongozi huyo wa upinzani kilichotokea siku ya Alhamisi wiki iliyopita, kwamba kingeweza kuteteresha amani ya nchi hiyo.