Monday, June 14, 2021
Swahili > Habari > Maafisa wa jeshi wapandishwa vyeo na Rais Magufuli.

Maafisa wa jeshi wapandishwa vyeo na Rais Magufuli.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amewapandisha vyeo maafisa wanne wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) na kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP)

Pia, Dkt. Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wengine watano katika Jeshi hilo kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).

Barua kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-IKULU, kwenda kwa vyombo vya habari.

Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka DCP na kuwa CP ni, Hamis Ngarama , Tusekile Mwaisabila , Augustine Sangalali Mboje na Gideon Marco Nkana .
Na Maafisa waliopandishwa vyeo kutoka SACP na kuwa DCP ni, Julius Mayenga Sang’udi , Afwilile Mwakijungu , John William Masunga , Phaustine Marint Kasike na Joram Yoram Katungi .