Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Lembeli aikacha Chadema, siasa si rafiki tena !

Lembeli aikacha Chadema, siasa si rafiki tena !

Kada wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, James Lembeli ametangaza kuachana rasmi na siasa za majukwaani na akijiuzulu uanachama wake ndani ya chama hicho.
Lembeli ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu akitokea CCM, ametangaza azma yake hiyo na kusema imechangiwa na mitikisiko inayokumbana nayo familia yake pamoja na yeye mwenyewe.

” Kuna taasisi ambazo nafanya nazo kazi ndizo zimeniambia kuwa nichague moja kushirikiana nao au kuendelea na siasa, ndipo nikaamua kuweka siasa pembeni na kufanya shughuli zangu,” amesema Lembeli.

James Lembeli, akijinadi jukwaani mwaka 2015 alipokua akigombea kiti cha Ubunge jimbo la Kahama Mjini.

Amesema, hali ilivyo sasa ni tofauti na alivyokuwa CCM na kuongeza kuwa, tangu ajiunge na CHADEMA kuna watu hawaendi kuzuru kwenye kaburi la marehemu Baba yake ambaye alikuwa ni mtemi hivyo ameona ni vyema akae pembeni na kuachana na siasa ili kuendelea kushirikiana katika mambo ya jamii.