Swahili > Kuhusu Sisi

Kuhusu Sisi

The East African Tribune ni gazeti linalopatikana kwa njia ya mtandao. Habari zake nyingi ni kuhusu mambo ya kisiasa, kijamii, michezo na kiuchumi katika eneo la Afrika Mashariki na maeneo yanayopakana na nchi za Afrika Mashariki na duniani kwa jumla.

Waanzilishi wa mtandao huu, ni waandishi wa habari kutoka eneo hili ambapo kwa kiasi fulani, wameona kuna haja ya kuwa na chombo ambacho mbali na kutoa habari lakini pia kitatoa ajira na kuwajengea uwezo waandishi wachanga katika tasnia.

Tunaamini kwamba, kutokana na kasi ya mitandao ya kijamii, mtandao wa East African Tribune utaweza kuleta chachu ya maendeleo katika sekta mbalimbali katika eneo hili ikiwemo biashara, utalii, kilimo na kuendelea.