Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Kizimbani kwa tuhuma za ubakaji.

Kizimbani kwa tuhuma za ubakaji.

Mkazi wa Kinondoni, Mashaka Komba (20), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es salaam kwa tuhuma za ubakaji.

Akisomewa shitaka jana mbele ya Hakimu Isaya Kasako na Mwendesha Mashtaka Grace Lwila, alidaiwa kuwa Juni 1, mwaka huu huko maeneo ya Kinondoni Hananasifu, alimbaka binti wa miaka 18(jina limehifadhiwa).

Baada ya kusomewa shtaka lake, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo.
Hakimu Kasako alisema dhamana ya mshtakiwa ipo wazi, awe na wadhamini wawili na bondi ya maandishi ya Tsh. milioni saba na kila mmoja kutoa nusu ya kiasi hicho cha fedha.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa mahabusu hadi Julai 16, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.