Tuesday, July 27, 2021
Swahili > Habari > Katiba mpya kuzinduliwa alhamisi nchini Burundi.

Katiba mpya kuzinduliwa alhamisi nchini Burundi.

Wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato mzima wa ubadilishaji katiba nchi ya Burundi, kwamba haukuzingatia sheria na katiba mpya inanuwia kumbakiza madarakani Rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.

Taarifa ya Ikulu ya Burundi imethibitisha kuwa sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa raia zitafanyika kesho siku ya alhamisi, saba katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la Bugendana ambako huko ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba, lakini pia kampeni ya chama kilichopo madarakani CN DD/FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.

Raia wa Burundi siku waliyopiga kura ya ndio kuipitisha katiba mpya.

Aidhaa taarifa hiyo ya Ikulu imetoa mwaliko kwa magavana wote na Wakuu wa tarafa za Burundi kushiriki kwenye sherehe hizo. Wamealikwa pia wawakilishi wa vyama vya kisiasa , asasi za kiraia pamoja na Viongozi wa kidini .

Ni hivi majuzi tu Umoja wa mataifa, na baadhi ya nchi za magharibi washirika wa zamani wa Burundi kama Ufaransa na Ubelgiji walikemea vikali mchakato mzima wa katiba kwa madai kua uligubiikwa na dosari nyingi na kwamba katiba hiyo mpya inatishia hata maridhiano ya kitaifa na uwakilishi wa makabila kwa Mujibu wa Mkataba wa Amani wa Arusha. Madai ambayo yamepingwa vikali na Wakuu wa Burundi.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, alipokua akipiga kura ya ndio kupitisha katiba mpya ya nchi hiyo itakayomuweka madarakani hadi mwaka 2034.

Katiba hii mpya ambayo inaanza kutekelezwa siku ya Alhamis itageuza mambo mengi kwenye taasisi za Kitaifa , lakini pia kutoa fursa kwa Katiba hii mpya ambayo itaanza kutekelezwa siku ya Alhamis itageuza mambo mengi kwenye taasisi za Kitaifa , lakini pia kutoa fursa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka wa 2034.