Friday, August 14, 2020
Swahili > michezo > Kane aibeba Uingereza, Kombe la Dunia 2018 – Urusi.

Kane aibeba Uingereza, Kombe la Dunia 2018 – Urusi.

Mshambuliaji Herry Kane, ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza, ameiongoza vyema timu yake ya Taifa kwenye mchezo wa kundi G uliopigwa usiku wa jana kuamkia leo dhidi ya timu ya Taifa ya Tunisia katika michuano ya Kombe la Dunia – 2018, nchini Urusi.

Mnamo dakika ya 11 kipindi cha kwanza, Kane aliipatia Uingereza goli la kuongoza .
Ferjani Sassi, aliisawazishia Tunisia kupitia mkwaju wa penati katika dakika ya 35
Kane, alirudi tena langoni mwa timu ya Tunisia kunako dakika ya 90 na kupachika goli la pili lililoipa ushindi timu ya Uingereza.

Mshambuliaji wa Tunisia, Ferjan Sassi akishangilia goli alilofunga  la kusawadhisha.

Kundi G, linaongozwa na timu ya Ubelgiji kwa pointi 3, Uingereza ikiwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 3 huku timu hizi zikiachana tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Tunisia wapo nafasi ya 3, na nafasi ya 4 imekaliwa na timu ya Taifa ya Panama .
Tunisia na Panama, wanatofautiana magoli ya kufunga na kufungwa, Tunisia wamefunga goli 1 na kufungwa magoli 2, huku Panama wakiwa hawana goli la kufunga na wamefungwa magoli 3.