Monday, January 18, 2021
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Jengo lashika moto Kariakoo.

Jengo lashika moto Kariakoo.

Moto mkubwa umeibuka Kariakoo katika Mtaa wa Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Vikosi kadhaa vya Jeshi la uokoaji na zimamoto vimefika  eneo la tukio kukabiliana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo hilo la ghorofa ambalo lina maduka mengi katika ghorofa ya chini.

Askali wa jeshi la uokoaji na zimamoto wakiendelea na harakati za kuzima moto huo katika jengo.

Jitihada za kuuzima moto huo zinafanywa na Jeshi la uokoaji na zimamoto likishirikiana na wananchi waliopo katika eneo la tukio maeneo ya Kariakoo.