Friday, August 14, 2020
Swahili > michezo > Hispania yafungasha vilago Kombe la Dunia.

Hispania yafungasha vilago Kombe la Dunia.

Timu ya taifa ya Uhispania leo imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kipigo cha magoli 4-3 kwa mikwaju ya penati , baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na timu ya taifa ya Urusi.

Penati za Hispania zimecheza na Pique, Iniesta, Ramos ambao wote wamefunga huku Koke na Iago Aspas wakikosa penati zao.

Urusi, hawajakosa penati hata moja, walifunga penati nne na kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi duniani katika mchezo wa mpira wa miguu.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Urusi wakishangilia baada ya kufuzu hatua ya 16 bora kwenda robo fainali.

Hispania sasa inaungana na Argentina na Ureno kwa kutolewa katika hatua ya 16 bora ya kombe la dunia 2018.