Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > habari > Harakati za kumsaka Rais wa kwanza mwanamke zaanza nchini Kenya.

Harakati za kumsaka Rais wa kwanza mwanamke zaanza nchini Kenya.

Huku juhudi za kisiasa pamoja na zile za kisheria kuleta usawa wa kijinsia kupitia kuwa na wanawake wengi katika nyadhifa za juu zikiendelea duniani, kipindi kimoja cha runinga kimeanza nchini Kenya kikiwa na lengo la kuendeleza mjadala huo mbele, kupitia ajenda ya ‘wanawake kama viongozi’ kwa lengo la kukuza usawa wa kijinsia na viongozi wanawake.

Kipindi hicho kwa jina ” Bi rais ” chenye sehemu 26, na kitatayarishwa na Media Focus on Africa kupitia ufadhili wa Muungano wa Ulaya na kitashirikisha wanawake wenye vipaji vya uongozi kwa lengo la kuongeza uwezo wao kuchukua nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini humo.

Frenny Jowi-Afisa wa mradi wa ” Bi rais ” Media Focus on Africa.

”Hatutafuti malkia wa urembo, tunatafuta wanawake ambao ni viongozi”. Sio kuwaleta wanawake katika runinga bali kuwafunza na kuwashauri”, alisema afisa wa mradi huo katika Media Focus on Africa, Frenny Jowi.

Watakaofuzu watapewa mafunzi ya uongoizi na ushauri ikiwa ni pamoja na mpango wa kuleta amani utakaoonyesha kwamba wanawake wanaweza kuchukua jukumu la kuzuia kuenea kwa uchochezi wa ghasia.

”Mwanamke atakayefaulu kushiriki katika kipindi hiki atakuwa mfano wetu sote.Tungependa kufanya kazi na wanawake wote watakaotuma maombi yao katika kipindi hicho kama wizara ya Jinsia”, alisema Lydia Mathia mshauri wa waziri wa Huduma kwa umma ,vijana na Jinsia.

Lydia Mathia, mshauri wa waziri wa Huduma kwa umma ,vijana na Jinsia.

Licha ya kuwa na sheria nzuri zinazotoa fursa ya usawa wa uwakilishi wa wanawake, vijana, walemavu na walio wachache, Kenya bado imesalia nyuma ikilinganishwa na mataifa mengine ya bara Afrika katika kuwa na wanawake katika nyadhfa mbali mbali za uongozi.