Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Boeing 787-8 Dreamliner yawasili Tanzania.

Boeing 787-8 Dreamliner yawasili Tanzania.

Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imewasili nchini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaongoza watanzania na wageni mbalimbali katika sherehe ya mapokezi ya ndege hiyo.
Ndege hiyo imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ikitokea mjini Seattle Marekani.

Rais Magufuli akiipokea ndega aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilipowasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ina uwezo wa kubeba abiria 262. Ndege nyingine ambazo zilinunuliwa na serikali ya Tanzania ni ndege moja aina ya Bombardier Q400 Dash 8 NextGen , ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 .
Rais Magufuli aliahidi kwamba, shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Viongozi mbalimbali walipowasili ili kuipokea ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilipowasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere- Jijini Dar Es Salaam.

Mbali na kuleta vigezo vya ndege kubwa katika ndege za wastani, 787 Dreamliner italipatia shirika la ndege la Air Tanzania ufanisi wa mafuta na mazingira ya utendaji, kwa kutumia chini ya asilimia 20 hadi 25 ya mafuta na asilimia 20 hadi 25 ya uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa ndege nyengine zilizotumika awali.