Friday, August 14, 2020
Swahili > Habari > Habari za kimataifa > Bangi yahalalishwa Canada.

Bangi yahalalishwa Canada.

Nchi ya Canada, imepitisha sheria inayoruhusu matumizi ya bangi, Sheria hiyo ilishinda kwa kupata kura za ndiyo kwa 52% zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani, huku 29% ya kura za maseneta zikisema hapana.
Sheria hiyo inasimamia udhibiti,usambazaji na uuzaji wake, Kwa sheria hiyo sasa raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria mwaka 2001.

Kutokana na kupitishwa kwa sheria hiyo sasa itawachukua majimbo,Manispaa na mamlaka takribani wiki kati ya nane hadi 12 kutengeneza masoko mapya ya kuuza bangi.
Pia, muda huu kabla ya kuanza kutumika kwa bangi rasmi, Polisi wataandaa mifumo mipya ya kisheria.
Kwa mjibu wa sheria hii mpya, mtu ataruhusiwa kuagiza bidhaa hiyo ya bangi kwa mfumo wa kimtandao kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika kisheria, Watu wazima wataruhusiwa kumiliki hadharani hadi gram 30 ya bangi kavu.

Mtu akivuta bangi.

Umri unaoruhusiwa kununua na kutumia bangi uliopitishwa kwa mjibu wa sharia hiyo ni kuanzia miaka 18, lakini baadhi ya majimbo yamependekeza umri wa kuanzia uwe ni miaka 19.