Monday, January 18, 2021
Swahili > Habari > Habari za kitaifa > Baba mzazi wa Marehemu Patrick bado kizungumkuti !

Baba mzazi wa Marehemu Patrick bado kizungumkuti !

Sakata la nani baba mzazi wa mtoto, marehemu Patrick aliyefariki usiku wa juzi Jijini Nairobi nchini Kenya, alipokuwa amelazwa katika hospitali moja akiendelea na matibabu, limechukua sura nyingine baada ya mtu anayefahamika kwa jina la Peter Cosovo kudai yeye ndiye baba mzazi wa mtoto Patrick.

Cheti cha ndoa ya Peter Cosovo na Rose ( Muna Love ), kilichotolewa kama ushahidi.

Cosovo, amesema hayo huku akiambatanisha picha waliyopiga yeye na Rose ( Muna Love ) wakati marehemu Patrick akiwa mdogo na cheti cha ndoa aliyofunga na Rose mwaka 2010 katika Kanisa La St.Peters la jijini Dar es salaam kama ushahidi wa yeye kuwa baba mzazi wa mtoto huyo.

Picha ya Peter na Rose ( Muna Love ) wakiwa na Marehemu Patrick wakati mdogo.

Mpaka sasa bado utata wa nani baba mzazi wa mtoto huyo haujatatuliwa, ingawa taarifa za mwanzo zinaeleza kuwa baba mzazai wa marehemu Patrick ni Castor Dickson, Mtangazaji wa kituo kimoja cha runinga hapa nchini.

Castor Dickson, Mtangazaji wa kituo cha runinga nchini, anayedaiwa kuwa baba mzazi wa marehemu Patrick.