Friday, August 14, 2020

Wimbi la hivi karibuni la kuuliwa kwa viongozi katika taasisi mbalimbali za serikali na Bunge limemsikitishaa na kumshtua Rais Yoweri Museveni ambapo ameagiza wabunge walindwe.

Rais ametangaza hayo baada ya kuwa na kikao na mhimili huo wa bunge na kukubaliana kuwa ili kuzuia mauaji ya viongozi jeshi la nchi hiyo, (UPDF) litoe ulinzi kwa watunga sheria hao.

Bunge la Uganda.

Katika kikao na Rais, wabunge wengi walieleza hofu zao kutokana na kile kilichotokea Juni 8 ambapo Mbunge wa Arua, Ibrahim Abiriga aliuawa na watu wasiojulikana na kumweleza Museveni kuwa baadhi yao wamepokea ujumbe wa vitisho kupitia mitandao ya kijamii.

Jenerali David Muhoozi-Mkuu wa Majeshi Uganda.

Baada ya kikao hicho, museveni alimwelekeza Mkuu wa Majeshi Jenerali David Muhoozi kukutana na Mkuu wa polisi bungeni pamoja na Anabella Nyamahoro ili kufanikisha ulinzi kwa wabunge wote.