Friday, August 14, 2020

Alhamisi ya leo, Juni 28, 2018 majira ya saa tano asubuhi Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amewasili katika uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Rais Mnangagwa, ambaye atakua nchini kwa muda wa siku mbili, baada ya kutua na kupokelewa na mwenyeji wake amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la heshima.

Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliofika kumpokea rais huyo wa Zimbabwe ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi;  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba;  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, ambapo Baada ya mapokezi hayo ya uwanjani, marais  hao walielekea Ikulu kwa mazungumzo zaidi.

Akiwa nchiini, Rais Mnagangwa atakutana na Wazimbabwe waishio Tanzania na kutembelea maeneo ya harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.